Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani

Like
332
0
Monday, 26 March 2018
Global News

 

Jacob Zuma

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani mwezi Aprili kwa makosa 16 yakiwemo ya kutumia vibaya ofisi wakati akiwa madarakani na ufisadi.

Duru za habari nchini Afrika Kusini kusini likiwemo gazeti la News24 limeeleza kuwa Zuma atafikishwa kizimbani katika Mahakama Kuu mjini Durban tarehe 6 Aprili 2018 kwa makosa 16.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa bodi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo, Brigedia Hangwani Mulaudzi amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii watawasilisha barua kwa mawakili wa Zuma juu ya wito huo.

Mulaudzi amesema kuwa Zuma atakabiliwa na mashtaka makubwa 16 ambapo rushwa na Matumizi mabaya ya ofisi yanatajwa kuwa ni moja ya mashtaka yaliyopewa kipaumbele.

Imeelezwa kuwa Jacob Zuma alifanya malipo ya risiti 783 kiholela, kwenye ununuzi wa silaha na vifaa vya jeshi nchini Afrika Kusini ambapo inakadiriwa kuwa ametumia mabilioni ya fedha kwenye ununuzi huo.

Mwaka 2012, Zuma aliingia kwenye kashfa nzito baada ya kutengeneza nyumba yake ya kifahari kwa kutumia fedha za serikali, ambapo alitumia zaidi ya dola milioni 25 za kimarekani.

Hata hivyo, kashfa hiyo ilitetewa na baadhi ya wabunge wa chama tawala nchini humo ANC, ambapo walieleza kuwa ukarabati huo ulizingatia vigezo.

Mnamo Februari 14, 2018. Mzee Zuma alitangaza kung’atuka madarakani baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wanachama wa ANC na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu wake wa Rais, Cyril Ramaphosa.

Comments are closed.