Rais wa Marekani Donald amemuomba radhi kwa niaba ya raia wa Marekani Jaji mpya wa mahakama ya upeo Brett Kavanaugh kwa kile alichokiita kwamba ni kampeni chafu za kisiasa zilizolenga kuharibu sifa binafsi ya Brett kutokana na mambo ya uzushi na uongo.
Trump ameyasema hayo katika sherehe za kuapishwa kwa jaji huyo mkuu wa mahakama ya juu ya Marekani shughuli ambazo zimefanyika katika Ikulu ya white House. Hatua ya kumthibitisha bwana Kavanaugh katika uteuzi wake huo iligubikwa na kashfa za ukatili wa kingono anaodaiwa kuufanya mwaka 1980.
Rais Donald Trump tangu awali alisikia madai ya Chama cha Upinzani cha Democratic kupinga uteuzi wa Bwana Kavanaugh ambaye binafsi amemuita kuwa ni Jaji makini na ambaye hana jambo lolote baya alilolifanya isipokuwa hizo ni jitihada za kutaka kumchafua tu.
Kauli hii ya Rais Trump imekuja huku hiki kikiwa ni kiapo cha cha awali cha bwana Kavanaugh chini ya usimamizi wa Jaji aliyemaliza muda wake Anthony Kennedy huku akiwa amebakiwa na kiapo cha mwisho kutoka kwa Rais Donald Trump.