RAPA KEKO HUENDA AKAJITOA CHINI YA USIMAMIZI WA SONY

RAPA KEKO HUENDA AKAJITOA CHINI YA USIMAMIZI WA SONY

Like
334
0
Wednesday, 27 May 2015
Entertanment

Keko rapa kutokea Uganada ametangaza mpango wake wa kujiondoa kwenye kampuni katika kampuni inayomsimamia ya Sony Music Entertainment Africa and ROCKSTAR4000.

Rapa huyu amekuwa msanii wa kwanza kutokea nchini Uganda kupata deal ya kufanya albam mbalimbali pamoja na usimamizi wa moja kwa moja chini ya kampuni hiyo ya sony.

Kupitia mtandao wa twitter rapa huyu ameelezea maumivu yake kwakusema kwamba hakuweza kuapata nafasi ya kufanya mziki mzuri toka ajiunge na kampuni hiyo mwaka 2012.

Maamuzi yake yakutaka kujitoa yanakuja kutokana na kukosa usimamizi mzuri kumtangaza na kuingiza mapato kupitia muziki wake,

Rapa huyu ni miongoni mwa wasanii wakubwa afrika ambao wamebahatika kupata tuzo ikiwemo ile ya chanel o aliyoipata kupitia wimbo wake wa ‘How We Do It’ ambao ulitwaa tuzo katika kipengere cha most gifted East African Video

Miongoni mwa wasanii wanaosimamiwa na kampuni ya Sony ni Alicia Keys, P!nk, Usher, Christina Aguilera, Pitbull na Chris Brown.

 

 

 

Comments are closed.