RAPA WA SUDANI AFUNGIWA KUPANDA NDEGE ZA WESTJET CANADA BAADA YA KUTISHIA KUMTAFUNA MUHUDUMU

RAPA WA SUDANI AFUNGIWA KUPANDA NDEGE ZA WESTJET CANADA BAADA YA KUTISHIA KUMTAFUNA MUHUDUMU

Like
306
0
Wednesday, 18 March 2015
Entertanment

Kampuni ya usafiri wa anga ya nchini Canada WestJet imemfungia rapa kutokea Sudan Emmanuel Jal kutopanda ndege ya shirika lao WestJet katika maisha yote.

Hatua hiyo ya kampuni hiyo imekuja mara baada ya rapa huyo kumtishia mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo kuwa analeseni inayomruhusu kumtafuna binadamu hivyo anaweza kumtafuna muhudumu huyo iwapo hatampatia kitafunwa.

Shirika hilo la gharama nafuu ya usafiri wa anga limechapisha taarifa hiyo kwenye tovuti yao kwakuonyesha kuwa wamekwazika na rapa huyo ambae aliwahi kuwa mwanajeshi utotoni mwake.

Miongoni mwa maneno yaliyotolewa na kampuni hiyo ni kwamba

Tunatambua ni muda mrefu mtu huyu amekuwa akipambana na njaa kwenye maisha ya utoto wake lakini shirika hilo sio sehemu ya ugavi wa chakula kwani chakula wanachotoa ni kwa kiwango cha safari za wateja wao kutoka sehemu moja mpaka nyingine ambapo wanapofika wanakuwa na uwezo wa kuagiza vyakula

 “We understanding that the person in question had starved for many years when he was a child, but – to clarify some confusion that he may have – WestJet is not the World Food Programme (WFP) and the food we serve aboard is more than enough to get our normal passengers to their next destination where they can buy and eat as much as they can in the many restaurants when they arrive at their destination.”

Muhudumu huyo alifikishwa hospitali kwaajili ya kufanyiwa matibabu kiaakili na kimwili kufuatia kupata mshtuko baada ya tukio hilo

Jal pia amejibu kupitia ukurasa wake wa facebook kwakusema ilikuwa ni utani

Jal ameeleza kushangazwa kwake na maamuzi ya kampuni hiyo kwa maana yeye na wahudumu walikuwa kwenye hali ya utani kwani mmoja wa wahudumu hao alimjibu kama analeseni basi aanze kumtafuna yeye ni nyama yenye mchanganyo na tangawizi

This is crazy is this true or somebody is Joking I have been ban for life to fly west jet, we were having fun with each other on the plane were i crake a joke that i have a license to eat humans if i dont get a sandwitch one of the hostees said she is ginger beef so I can start with her and we all laugh loud read the article

 

Comments are closed.