REA KUMALIZA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI

REA KUMALIZA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI

Like
259
0
Tuesday, 06 January 2015
Local News

 ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini -REA Awamu ya Pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini -Tanesco unatarajiwa kukamilika, ikiwa ni pamoja na kuvipatia umeme Vijiji 1,500.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO kwa nyakati tofauti alipofanya ziara katika vijiji vya Ihale, Bukombe, Nyamikoma, Bushigwamala, Mwamagigisi, Mkula vilivyopo katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Profesa MUHONGO amefanya ziara katika Mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua Miradi ya Umeme Vijijini pamoja na kuzungumza na Wananchi.

Comments are closed.