IKIWA tayari mwelekeo unaonesha kuwa kinyang’anyiro cha kiti cha urais wa Marekni kitakuwa ni kati ya Bi. Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican, wazee na vigogo ndani ya chama cha Republican wamesema kuwa hawapo tayari kumruhusu Trump Agombee Urais.
Wakuu hao wa chama cha Republican wamesema ikiwa watamruhusu Donald Trump awe mgombea urais wao basi kuna uwezekano mkubwa wa chama chao kusambaratika.
Mmoja ya vigogo hao wa Republican, Seneta Lindsey Graham wa South Carolina amesema njia ya pekee ya kumzuia Donald Trump ni wanachama kumuunga mkono mgombea mwingine wa Republican Ted Cruz.