RIHANA AREJEA INSTAGRAM BAADA YA MIEZI SITA YA UKIMYA

RIHANA AREJEA INSTAGRAM BAADA YA MIEZI SITA YA UKIMYA

Like
461
0
Monday, 03 November 2014
Entertanment

Msanii kutoka marekani mzaliwa wa Saint Michael, huko  Barbados, mwaka 1988 February 20,  alifungiwa kuendelea kutumia mtandao wa instagram kwa takribani miezi sita mara baada ya kukiuka taratibu za mtandao huo.

miezi michache nyuma msanii huyo alipost picha yake kwenye akaunti ya Instagram akiwa hana top kuziba mwili wake sehem ya juu hivyo kumfanya kuwa mtupu picha alizopiga kwenye photoshoot ya jarida la Lui.

picha hiyo iliondolewa haraka na uongozi wa mtandao huo na akaunti yake ilifutwa kabisa baada ya muda mfupi lakini timu ya wataalamu wa mtandao huo walidai ilifutika kwa bahati mbaya na hivyo baadae waliirudisha tena.

Rihana hakuwahi kusema lolote kuhusiana na tukio hilo na badala yake aliacha kabisa kutumia mtandao huo

msanii huyo mwenye followers milion 12 amepokelewa kwa kishindo na mashabiki wake pamoja na mtandao wenyewe wa instagram

wasemaji wa mambo wanaamini kwamba huenda mtandao huo pia umemrudisha kwa kutambua ushawishi wake mkubwa alionao kwenye mtandao huo.

Rihanna-600x597

picha aliyopost baada ya miezi sita

Comments are closed.