RIO2016: WACHEZAJI KOREA KUSINI NA KASKAZINI WAJIPIGA SELFIE

RIO2016: WACHEZAJI KOREA KUSINI NA KASKAZINI WAJIPIGA SELFIE

Like
254
0
Tuesday, 09 August 2016
Slider

Wanamichezo wa mazoezi ya viungo kutoka Korea Kusini na Kaskazini, ambao wanashiriki Michezo ya Olimpiki Rio 2016, wameuonesha ulimwengu ishara ya umoja, kwa kupiga selfie pamoja.

Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Kaskazini walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.

Picha za wanawake hao wawili zimesifiwa sana kwa kuashiria moyo wa Olimpiki wa kuwaleta watu pamoja.

Korea Kaskazini na Kusini huwa na uhasama mkubwa.

Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umedorora hata zaidi, kutokana na hatua ya karibuni ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora.

Comments are closed.