RIPOTI YA MWISHO YA NDEGE YA MALAYSIA MH17 KUTOLEWA OCTOBA

RIPOTI YA MWISHO YA NDEGE YA MALAYSIA MH17 KUTOLEWA OCTOBA

Like
195
0
Friday, 28 August 2015
Local News

WACHUNGUZI wa Uholanzi wamesema ripoti ya mwisho kuhusu kuangushwa kwa ndege ya Malaysia MH17 katika anga ya mashariki mwa Ukraine mwaka uliyopita itatolewa Oktoba 13.
Bodi ya usalama ya Uholanzi imesema katika taarifa kuwa iliwafahamisha ndugu wa wahanga na wawakilishi walioruhusiwa kwenye uchunguzi wa chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo, juu ya tarehe ya kutolewa kwa ripoti hiyo.
Bodi hiyo imesema kabla ya kutolewa rasmi kwa ripoti hiyo, ndugu wa wahanga watafamishwa kuhusu ugunduzi wa uchunguzi huo katika mkutano wa siri.

Comments are closed.