RIPOTI ZA KUTATANISHA ZAWAKERA NDUGU WA ABIRIA WALIOKUWEMO KWENYE NDEGE YA MALAYSIA

RIPOTI ZA KUTATANISHA ZAWAKERA NDUGU WA ABIRIA WALIOKUWEMO KWENYE NDEGE YA MALAYSIA

Like
226
0
Friday, 07 August 2015
Global News

NDUGU na jamaa wa abiria waliokuwemo katika ndege ya Malaysia iliyotoweka, yenye namba za safari MH370 wameoneshwa kukasirishwa na kile wanachosema kuwa ripoti zinazotolewa juu ya kupotea kwa ndege hiyo ni za kutatanisha.

Jana Malaysia ilithibitisha kuwa kipande cha bawa la ndege kilichogunduliwa katika kisiwa cha Reunion kilikuwa ni sehemu ya ndege hiyo iliyopotea.

Hata hivyo nchi ya Ufaransa imesema itapeleka vifaa zaidi vya majini na angani nje ya kisiwa cha Reunion leo kutafuta mabaki zaidi ambapo jumla ya watu 239 walikuwa kwenye ndege hiyo iliyopotea saa moja baada ya kuanza safari yake mwezi Machi mwaka jana.

 

Comments are closed.