ROY KEANE: VAN GAAL APEWE MUDA KUKIJENGA KIKOSI IMARA

ROY KEANE: VAN GAAL APEWE MUDA KUKIJENGA KIKOSI IMARA

Like
288
0
Tuesday, 10 March 2015
Slider

Aliekuwa Captain wa Manchester United Roy Keane ameesema ni janga kubwa kwa klabu hiyo kushindwa kumaliza hatua ya nne bora ila anaamini kuwa meneja wa sasa wa timu hiyo Louis van Gaal anahitaji muda wa takribani miaka miwili ama mitatu kukijenga kikosi hicho.

Ndoto za klabu hiyo kwenye michuano ya FA zilifutika hapo jana baada kupokea kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa wapinzani wao wa jadi Arsenal katika robo fainali za michuano hiyo

Keane ameeleza kuwa si jambo la kushangaza kuona Van Gaal akikosolewa kwa sasa kufuatia mwenendo wa klabu hiyo ila apewe muda usiopungua miaka miwili au mitatu

Keane ambae ameshinda makombe saba ya ligi ya Uingereza, makombe menne ya FA na Champions ligi katika kipindi cha miaka 12 akiitumikia klabu hiyo tangu mwaka 1993 hadi 2005 alisema

“mashabiki wengi hawafahamu jinsi ya kuongoza klabu kubwa kama Manchester United  walipaswa kumpa muda David Moyes ila hawakufanya hivyo badala yake walimtimua na kumleta Van Gaal nae pia anahitaji kupewa muda kukijenga kikosi imara”

Alisema Keane wakati anahojiwa na kituo cha bbc juu ya mustakabari wa klabu hiyo ya Manchester United

Comments are closed.