RUSHWA: MAAFISA SITA WA FIFA WAKAMATWA

RUSHWA: MAAFISA SITA WA FIFA WAKAMATWA

Like
236
0
Wednesday, 27 May 2015
Slider

MAAFISA  sita wa ngazi ya juu wa shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA,wamekamatwa na maafisa wa vyombo vya sheria vya Uswisi hii leo mjini Zurich, siku mbili kabla ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo.

Maafisa hao wanakabiliwa na kitisho cha kuhamishiwa Marekani ambako watakabiliwa na madai ya kuhusika na visa vya udanganyifu, ukandamizaji, na kubadilisha fedha kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa idara ya sheria ya serikali kuu ya Uswisi,maafisa hao wa FIFA wanakabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya mamilioni ya dola tangu mwaka 1990 kutoka vyombo vya habari za spoti na kampuni ya zana za spoti.

Badala yake kampuni hizo zimemepatiwa ruhusa ya kuripoti, kusimamia na kushughulikia  masuala ya kibiashara katika michuano ya kabumbu nchini Marekani na Amerika ya kusini.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa Rais wa  FIFA, Joseph Blatter mwenye umri wa miaka 79 siyo miongoni mwa watuhumiwa na atapigania kuchaguliwa upya ijumaa ijayo kuliongoza shirikisho hilo la soka ulimwenguni.

 

Comments are closed.