RUSHWA: MAHAKIMU 20 WAFUKUZWA KAZI GHANA

RUSHWA: MAHAKIMU 20 WAFUKUZWA KAZI GHANA

Like
208
0
Tuesday, 08 December 2015
Global News

MAMLAKA ya mahakama nchini Ghana imewafuta kazi mahakimu 20 huku wengine wakiendelea kuchunguzwa kutokana na kuhusishwa na kashifa ya kupokea rushwa.

Ufisadi wa mahakimu hao umebainika baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Aremeyaw Anas, kukusanya kwa muda wa miaka miwili kanda za video zenye muda wa saa 500 kama ushahidi dhidi ya mahakimu 30.

Kutokana na sakata hilo, baadhi ya mahakimu nchini Ghana wametaka kuwepo kwa mabadiliko katika mahakama nchini humo ili kukomesha vitendo hivyo.

Comments are closed.