SAKASAKA 2016 INAKUPA NAFASI YA KUTWAA MILIONI TATU

SAKASAKA 2016 INAKUPA NAFASI YA KUTWAA MILIONI TATU

Like
398
0
Thursday, 09 June 2016
Local News

Baada ya kukabidhi magari mawili na pikipiki kumi kwa wasikilizaji wake kupitia

shindano la shikandinga , EFM redio inakuja na donge nono kupitia mchezo wa

sakasaka ambao huchezeshwa kila mwaka toka kituo kianzishwe.

Saka saka ni shindano ambalo efm redio huficha kitu katika eneo fulani ambapo  msikilizaji hupewa maelekezo yake hivyo atatakiwa kwenda katika eneo

hilo na kukitafuta hicho kitu kulingana na shindano.

Mwaka huu mchezo wa sakasaka utaanza tarehe 12/06/2016, utachezeshwa katika

wilaya tano (5) ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Mkuranga, na Kisarawe

ambapo jumla ya kiasi cha milioni tatu (3) kushindaniwa katika kila wilaya.

Ili kuweza kushiriki katika mchezo huu jamii inapaswa kusikiliza kwa makini

vipindi vya redio ambapo atapata dondoo za jinsi mchezo utavyokua ukichezwa

Lengo madhubuti la mchezo huu ni kusaidia jamii kwa namna moja au nyingine

kwani pesa ambazo watajishindia zitawasaidia katika maisha yao kiujumla kama

biashara, familia, elimu, n.k

“Idadi kubwa ya wasikilizaji wetu wana changamoto nyingi za maisha hivyo kama

redio tunawawezesha kwa kupitia vitu tofauti tofauti ambavyo vitawasaidia

kujikwamua kimaisha”

Comments are closed.