SAKATA LA KUSHAMBULIWA KWA ALIEKUWA MLINZI WA DK SLAA LACHUKUA SURA MPYA

SAKATA LA KUSHAMBULIWA KWA ALIEKUWA MLINZI WA DK SLAA LACHUKUA SURA MPYA

Like
310
0
Friday, 13 March 2015
Local News

SAKATA la kushambuliwa kwa aliyekuwa Mlinzi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dokta WILBROAD SLAA ,KHALID KAGENZI ,limechukua sura mpya baada ya kiongozi huyo kufika Katika kituo Kikuu Cha Polisi na kuandika maelezo takribani saa Tano.

Hivi karibuni Dokta SLAA kupitia kwa mmoja wa Viongozi wa CHADEMA,MABERE MARANDO, alidai kuwepo kwa mpango wa kumdhuru ambao unaratibiwa na Maofisa wa Usalama kwa kushirikiana na baadhi ya Viongozi wa CCM.

Mpango huo ulidaiwa kuwa ungetekelezwa kupitia kwa KAGENZI, ambaye baadaye aliteswa na kushambuliwa na wafuasi wa Chama hicho,ikiwa ni mkakati wa kumlazimisha kukiri.

Comments are closed.