RAIS wa Sudan kusini Salva Kiir amesisitiza nia yake ya kuendeleza makubaliano ya Amani yaliyotiwa saini mwezi Agosti, siku mbili baada ya serikali na waasi kushutumiana kwa kukiuka makubaliano hayo.
Rais Kiir ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba Sudan kusini inapaswa kufikia maridhiano na kufungua kurasa mpya na kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia nchi hiyo kutekeleza makubaliano ya amani.
Mvutano wa kuwania madaraka kati ya rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar uligeuka kuwa machafuko makubwa katikati ya mwezi Disemba mwaka 2013.