RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye amewasili nchini leo, anatarajiwa kutia saini mkataba wa kuiingiza rasmi nchi hiyo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kiir atatia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo baadaye.