WAKATI leo rais wa Sudan Salva Kiir akitarajia kusaini muafaka wa kugawana madaraka mjini Juba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza mbinyo kwa rais huyo, likionya kuwa liko tayari kuchukua hatua ya haraka ikiwa hatosaini muafaka wa kumaliza vita vilivyodumu miezi 20.
Rais Kiir anatarajiwa kusaini muafaka wa kugawana madaraka mjini Juba , pamoja na viongozi wa Kenya, Uganda, Sudan na Ethiopia, lakini msemaji wake amesema bado hajaridhishwa.
Kiongozi wa waasi Riek Machar alisaini makubaliano hayo wiki moja iliyopita mjini Addis Ababa.