SAMATTA MFUNGAJI BORA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA

SAMATTA MFUNGAJI BORA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA

Like
448
0
Monday, 09 November 2015
Slider

Klabu ya soka ya TP Mazembe, ya Jamuhuri ya Kidemocrasia ya Congo imetwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika.

TP Mazembe wakicheza kwao katika uwanja wa Stade du TP Mazembe Lubumbashi, waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi Union Sportive Medina d’Alger.

Mshambuliaji Mbwana Samatta ndiye aliyeanza kuifungia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 75 ya mchezo, kisha Roger Assale akahitimisha kazi kwa bao la pili katika dakika ya 90.

Mazembe imenyakua Ubingwa huu wa Afrika, ikiwa ni mara yao ya 5, kwa jumla ya Mabao 4-1 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali ya kwanza uliofanyika wiki iliyopita.

Bao la Samatta katika mchezo huo, limemfanya afikishe bao 7 msimu huu na kuibuka ndie mfungaji bora wa michuano hii.

Baada ya kutwaa taji hili, TP Mazembe wamezoa donge la dola 1.5 milioni na pia wataiwakilisha Afrika kwenye mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan mwezi Desemba.

Comments are closed.