MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.
Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma, Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Amesema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa