Waendesha mashtaka nchini Korea kusini wamevamia ofisi za kampuni ya kielektoniki ya Samsung kama sehemu ya uchunguzi wa sakata ya kisiasa inayomuhusu rais Park Geun-hye.
Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Samsung ilimpatia pesa mtoto wa kike wa Choi Soon-sil, ambaye ni rafiki wa karibu wa rais.
Bi Choi anashutumiwa kutumia urafiki wao kuingilia kati siasa na utoaji wa zabuni za kibiashara.
Samsung imeithibitishia BBC kuwa uvamizi huo ulifanyika ikisema “hakuna maelezo zaidi “.
Rais Park ameomba msamaha kwa uhusiano wa karibu na Bi Choi lakini anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu.