SAMSUNG NOTE 7 YASHIKA MOTO KWENYE NDEGE

SAMSUNG NOTE 7 YASHIKA MOTO KWENYE NDEGE

Like
240
0
Thursday, 06 October 2016
Slider

Simu ya kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7, ambayo ilikuwa imethibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, imeshika moto kwenye ndege nchini Marekani.

Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa na abiria aliyekuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines.

Shirika hilo limesema abiria waliokuwa kwenye ndege moja yake, iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland, waliondolewa kwenye ndege kwa dharura kabla ya ndege hiyo kupaa Jumatano.

Kampuni ya Samsung iliwashauri watu waliokuwa wamenunua simu za Note 7 kuzirejesha kwa kampuni hiyo baada ya kugunduliwa zilikuwa na tatizo kwenye betri zake.

Samsung imesema bado inachunguza kisa hicho cha Jumatano.

“Tunashirikiana na maafisa wa serikali na maafisa wa shirika la Southwest kupata simu hiyo na kuthibitisha chanzo (cha moto huo),” kampuni hiyo imesema kupitia taarifa.

Msemaji mmoja wa shirika la Southwest Airlines amemabia BBC: “Abiria mmoja alitufahamisha kuhusu moto uliokuwa unafuka kutoka kwa simu. Abiria wote na wahudumu wa ndege waliondolewa salama kutoka kwenye ndege.”

Mmiliki wa simu hiyo Brian Green, akizungumza na Jordan Golson wa shirika la The Verge, amesema alinunua simu hiyo tarehe 21 Septemba.

Amesema simu hiyo ilikuwa na alama ya mraba ya rangi nyeusi kwenye pakiti yake, alama ambayo iliongezwa na Samsung kutofautisha kati ya simu zilizokuwa zimeuzwa awali ambazo zilidaiwa kutokuwa salama na simu mpya zilizokuwa zimechunguzwa.

Comments are closed.