SAVE THE CHILDREN YAWAKUTANISHA WATOTO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KWA AJILI YA KUSIKILIZA MAONI YAO

SAVE THE CHILDREN YAWAKUTANISHA WATOTO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KWA AJILI YA KUSIKILIZA MAONI YAO

Like
271
0
Tuesday, 26 May 2015
Local News

SHIRIKA la kimataifa la kuhudumia watoto la Save the children leo limewakutanisha watoto pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa nchini kwa ajili ya kusikiliza maoni ya watoto hao ili kuingiza katika ilani zao za uchaguzi pamoja na kutoa tamko la watakachofanya baada ya miaka 5 ijayo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam amesema kuwa kwa sasa wanafanya utaratibu wa kukutana na vyama vya Siasa ambavyo vimeshiriki katika mchakato wa uchaguzi na kuweza kuchukua maeneo 10 ambayo watoto wameyataja kuwa ni muhimu kuzingatiwa katika ilani ya uchaguzi.

Aidha amesema kuwa kumekuwa na tatizo la mimba za utotoni kwa watoto lakini limeonekana kutotiliwa mkazo kutokana na Serikali kushindwa kuweka sheria madhubuti itakayodhibiti tatizo hilo.

2

4

Comments are closed.