SAVE VULNERABLE FOUNDATION KUSAIDIA WANANCHI WAISHIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

SAVE VULNERABLE FOUNDATION KUSAIDIA WANANCHI WAISHIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

Like
377
0
Wednesday, 04 March 2015
Local News

 SHIRIKA  lisilo  la Kiserikali  la  Save  Vulnerable  foundation  linatarajia    kuanzisha  mradi  utakao wasaidia  wananchi  wa Mjini na Vijijini  wanaoishi  katika  mazingira  magumu,huku waliwalenga Zaidi watu wenye  matatizo ya  Ulemavu  katika suala la Elimu

Akizungumza na Waandishi  wa Habari  Jijini  Dar es salaam Katibu Mkuu wa Shirika  hilo  LEONTINE  RWECHUNGURA  amesema kuwa  ripoti ya haki za Binadamu  ya mwaka  2010  na Ripoti ya Tanzania  ya  mwaka 2008 imethibitisha  kuwa  kiwango cha  sasa  cha Ujinga  kwa watu  wenye Ulemavu  nchini ni  Asilimia 47 nukta 6 ikilinganishwa na Asilimia  25 nukta 3,  ambao hawana Ulemavu  ambayo imeonyesha nusu ya watu wenye Ulemavu nchini  hawapati Elimu kama  inavyo stahili.

RWECHUNGURA  amebainisha kuwa  mradi huo utaanza  katika  shule za Msingi na Sekondari  ambazo ni  Jangwani,  Pugu, na  Benjamini  Mkapa ikiwemo shule ya Uhuru Mchanganyiko.

SAV2 SAV3 SAV4

 

 

 

Comments are closed.