IMEELEZWA kuwa sekta ya mifugo nchini haichangii uchumi wa nchi kama ilivyotarajiwa na serikali.
Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa maaandalizi ya mpango mkakati wa sekta ya mifugo, Naibu Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mheshimiwa WILLIAM OLE NASHA, amesema kutokana na hali hiyo Serikali inakusudia kuandaa mkakati ambao utainua sekta hiyo nakuweza kuchangia uchumi wa nchi na wananchi na wananchi kwa ujumla.
Amesema kuwa pamoja na Tanzania kuwa nchi ya tatu Afrika kwakuwa na mifugo mingi ,lakini bado sekta hiyo haijachangia katika maendeleo ya Taifa.