SENEGAL: KESI YA HABRE YAAHIRISHWA

SENEGAL: KESI YA HABRE YAAHIRISHWA

Like
173
0
Tuesday, 21 July 2015
Global News

KESI ya kihistoria dhidi ya Kiongozi wa zamani wa Chad Hissene Habre iliyokuwa imerejeshwa mahakamani leo nchini Senegal sasa imeahirishwa hadi mwezi Septemba mwaka huu.

Mahakama imetoa muda huo kwa wakili wapya wa kiongozi huyo wa zamani wa kimila kujiandaa kwa kesi inayomkabili ya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili na uhalifu wa kivita.

Habre ambaye amekataa kuitambua mahakama hiyo alikataa kuzungumza mahakamani huku akiwashauri wakili wake wasimwakilishe mahakamani hatua iliyomlazimu hakimu kuingilia kati na kushurutisha apewe mawakili wapya.

H2

 

Comments are closed.