SENETA wa Nebraska- Ben Sasse amesema hatamuunga mkono mgombea urais anayeongoza miongoni mwa wagombea wa chama cha Republican Donald Trump.
Sasse ndiye mwanachama wa kwanza wa ngazi ya juu wa chama cha Republican aliyejitokeza kutangaza hadharani kwamba hatamuunga mkono Trump.
Amesema amesikitishwa sana na kuvunjwa moyo na mfanyabiashara huyo na kwamba atamtafuta mgombea mwingine wa kumuunga mkono iwapo Trump atashinda uteuzi wa Republican.