SERENGETI BOYS DIMBANI TAIFA LEO

SERENGETI BOYS DIMBANI TAIFA LEO

Like
578
0
Tuesday, 21 August 2018
Sports

Michuano ya vijana walio chini ya miaka 17 inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaa kufuzu fainali za Afcon leo Tanzania (Serengeti Boys ) watakuwa dimbani dhidi ya Rwanda (Amavubi Junior )vijana wa Kagame katika mchezo ambao utatoa matokeo ya nani atakuwa kinara katika kundi A.

Mpaka sasa Rwanda na Tanzania zimetinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ikiwa Tanzania ndio inaongoza kundi hilo kwa idadi ya magoli ya kufunga ,katika Kundi B Burundi na Sudani tayari zimeyaaga mashindano hayo.

Wenyeji Serengeti Boys walianza vyema michuano hiyo ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Burundi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam huku Rwanda wakianza kwa kuifunga Sudan mabao 3-1 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Tanzania kupitia vijana wa Serengeti Boys ndio mabingwa wa Kombe la Vijana la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati Cecafa wa mwaka 2017, walitwaa ubingwa baada ya kuwalaza Somalia mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezewa mjini Bujumbura, Burundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *