SERIKALI YA MAREKANI YAMTUHUMU NETANYAHU KUKIUKA MPANGO WA AMANI

SERIKALI YA MAREKANI YAMTUHUMU NETANYAHU KUKIUKA MPANGO WA AMANI

Like
233
0
Friday, 20 March 2015
Global News

MSEMAJI wa Serikali ya Marekani, JOSH EARNEST, amesema Waziri Mkuu wa Israel BENJAMIN NETANYAHU, amekiuka dhamira yake ya awali ya kuundwa kwa Mataifa mawili kama suluhu ya mgogoro wa Israel na Palestina mwanzoni mwa wiki hii.

Matamshi ya waziri mkuu huyo wa Israel ya kutotaka kuwepo kwa taifa la Palestina yanaonekana na wengi kama ndio yaliyomsaidia kushinda katika uchaguzi uliofanyika siku March 17 mwaka huu.

Taarifa zinasema kuwa NETANYAHU amekiambia Kituo cha Televisheni cha Marekani, MSNBC, kwamba bado anabaki na dhamira ya kuundwa kwa Taifa la Wapalestina, huku akikana taarifa za kubadili msimamo katika sera yake.

Comments are closed.