WANANCHI wa kata ya Makumbusho wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam wameilalamikia serikali ya mtaa wa Kambangwa kwa kitendo cha watendaji hao kujichukulia sheria mkononi ya kuwatoza faini juu ya matumizi ya huduma za kijamii ambazo kwa mujibu wa halmashauri huduma hizo hutolewa bure.
Aidha wanachi hao wameshindwa kufahamu mapato na matumizi ya ofisi ya serikali yao kutokana na kutoitwa katika vikao tangu kupatikana kwa uongozi mpya mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na kituo hiki jijini hapa mwenyekiti wa mtaa huo Dadson Gama amekiri kupata malalamiko hayo na kubainisha kuwa sababu za kutofanyik kwa vikao kuwa ni uzembe wa viongozi.