SERIAKALI YAAHIDI KUTETEA WANYONGE DHIDI YA VITENDO VYA DHULUMA KWENYE ARDHI, VIWANJA, MAJENGO NA MASHAMBA

SERIAKALI YAAHIDI KUTETEA WANYONGE DHIDI YA VITENDO VYA DHULUMA KWENYE ARDHI, VIWANJA, MAJENGO NA MASHAMBA

Like
339
0
Wednesday, 04 February 2015
Local News

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa WILLIAM LUKUVI amesema Serikali itahakikisha inapambana na watu wote wanaoendesha vitendo vya dhuluma, matapeli na wanaonyang’anya viwanja, majengo, mashamba na ardhi za wanyonge.

Waziri LUKUVI ametangaza azma hiyo wakati akijibu baadhi ya hoja za Wabunge waliochangia Taarifa ya Kamati ya Bunge, ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyowasilishwa na kupitishwa Bungeni mjini Dodoma.

Amebainisha kuwa anatambua kwamba hasa maeneo ya mijini kuna dhuluma nyingi zinafanyika ambapo Masikini, Yatima na Wajane wanadhulumiwa na kunyang’anywa ardhi na majengo yao.

 

Comments are closed.