SERIKALI imekifungia Kiwanda cha TWIGA Cement kilichopo Wazo hill jijini dare s salaam baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi wanaoishi eneo hilo kuvuta hewa chafu inayotoka katika kiwanda hicho na kukitaka kulipa faini ya shilingi milioni 50. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dare s salaam Mwanasheria wa mazingira wa NEMC amesema kuwa kumekuwa na malamiko ya muda mrefu na hivyo Serikali wameutaka uongozi wa kiwanda hicho cha Twiga Cement kukifunga ili kuweza kurekebisha mazingira ya watu wanaoishi katika eneo hilo. Hapo jana EFM iliripoti kuhusiana na Tatizo hilo, ambapo Mkurugenzi wa Kiwanda hicho bwana ALFONSO RODRIGUEZ alisema kuwa wapo mbioni kuhakikisha wanarekebisha hali hiyo ili kuondoa adha hiyo kwa wananchi wa eneo hilo.