SERIKALI imeombwa kuboresha maslahi ya Walimu wanaofundisha Elimu maalumu kama vile Wasiosikia na Wasiiona, ili walimu wengi wanaomaliza vyuoni wawe na ari ya kuweza kwenda kufundisha katika shule hizo.
Rai hiyo imetolewa Jijin Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mugabe Kitengo Wasiosikia ,PHILBETH ANDREW wakati akizungumza na Efm ofisini kwake.
Amesema endapo Serikali itaona umuhimu na kuamua kulitilia mkazo suala hilo, itaweza kuondoa upungufu wa Walimu katika shule za Elimu maalum.