SERIKALI imeombwa kulipatia Hati Miliki soko la Ndizi na Matunda lililopo mabibo urafiki jijini dar es salaam kutokana na soko hilo kukosa ufadhili wa mikopo katika benki kwa sababu ya kukosa hati hiyo.
Akizungumza na Efm Mwenyenye kiti wa Soko hilo Bwana KIBWANA ALFAN PAZI amesema kuwa endapo watapata hati miliki ya soko hilo itawasaidia kupata wafadhili kutoka sehemu mbalimbali watakao wawezesha katika biashara yao.
PAZI amebainisha kuwa vijana wengi wameweza kujiajili wenyewe kupitia nafasi wanazo zipata katika masoko na kuweza kujikimu katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kuondokana na makundi ya ukabaji kwa ajili ya kupata pesa.