SERIKALI IMEOMBWA KUREKEBISHA BARABARA INAYOELEKEA KWENYE KITUO CHA MAWASILIANO

SERIKALI IMEOMBWA KUREKEBISHA BARABARA INAYOELEKEA KWENYE KITUO CHA MAWASILIANO

Like
250
0
Monday, 21 September 2015
Local News

MADEREVA wa Mabasi Jijini Dar es salaam wanaotumia kituo cha daladala cha Mawasiliano wameiomba serikali kuboresha Barabara ya Kuelekea Kituoni hapo ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa magari.

Wakizungumza na Efm radio baadhi ya Madereva wanaotumia Kituo hicho wamesema kuwa Ubovu wa Barabara hiyo ni tatizo la Kipindi Kirefu ambalo bado halijapatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni MUSSA NATTY amebainisha kuwa serikali inatambua tatizo la barabara hiyo na kuwa kwa kushirikiana na benki ya dunia wameandaa mradi ambao utahusika kuboresha miundombinu ya jiji la Dare s salaam.

Comments are closed.