SERIKALI IMEOMBWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA JUHUDI ZA KIMAENDELEO ZINAZOFANYWA NA MTANDAO WA WASANII

SERIKALI IMEOMBWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA JUHUDI ZA KIMAENDELEO ZINAZOFANYWA NA MTANDAO WA WASANII

Like
272
0
Wednesday, 18 March 2015
Local News

SERIKALI  imeombwa kutoa ushirikiano katika juhudi mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na Mtandao wa wasanii Tanzania kwa lengo la kuimarisha maisha ya wasanii,wanamichezo na wanahabari kote nchini.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Mtandao wa wasanii Tanzania Casim Taalib alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana  katika mtandao huo tangu uanzishwe miaka 10 iliyopita.

Taalib amesema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kujenga nyumba 104 za wanachama wake  katika eneo la Ekari 800 lililopo Mwandege Mkuranga.

Comments are closed.