SERIKALI IMESEMA HAINA KUHATARISHA USALAMA WA WANAHABARI

SERIKALI IMESEMA HAINA KUHATARISHA USALAMA WA WANAHABARI

Like
281
0
Wednesday, 25 November 2015
Local News

SERIKALI imesema haijawahi, haina na haitokuwa na nia yeyote ile ya kuhatarisha usalama wa Wanahabari na kuwa ni jambo la maana kujenga mahusiano mazuri ya kuaminiana baina ya Serikali na Wadau wa habari kwa kuwa pale ambapo uaminifu unakosekana ndipo hisia na dhana potofu zinapojitokeza.

Akizungumza na Efm leo jijini Dar es salaam  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Elisante Olegabriel amesema kuwa sekta ya habari ni  muhimu  kwa kuwa inabeba sekta zingine zote za Taifa hivyo Wanahabari na Wadau wa habari nchini wanatakiwa kuzingatia weledi, kanuni na maadili ya kazi ili kutopoteza imani yao kwa Wananchi na Serikali.

Comments are closed.