SERIKALI IMETAKIWA KUTOA RATIBA SAHIHI YA MFUMO WA UANDIKISHAJI WA BVR

SERIKALI IMETAKIWA KUTOA RATIBA SAHIHI YA MFUMO WA UANDIKISHAJI WA BVR

Like
285
0
Thursday, 19 February 2015
Local News

 MTANDAO wa Asasi za Kiraia wa kuangalia Chaguzi Tanzania -TACCEO unaoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu umeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa ratiba sahihi ya jinsi zoezi la Uandikishaji wa wapiga Kura kwa Mfumo wa BVR litakaloendeshwa nchi nzima linatarajiwa kukamilika lini ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Mtandao huo MARTINA KABISAMA amesema kuwa mtandao huo ambao unatarajia kutuma waangalizi Zaidi ya 100 nchi nzima kwa ajili ya kuangalia Uandikishwaji wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa BVR katika Wilaya zote za Tanzania Bara.

Amesema madhumuni ya uangalizi huo ni kushuhudia ni kwa kiasi gani wale walio pembeni hasa jamii za wafugaji na waokota matunda wanashirikishwa na kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Comments are closed.