SERIKALI imetakiwa kuhakikisha inatunga na kuboresha sera za kupambana na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake katika masoko na maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Kituo cha Usuluhisho cha Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA, Gladness Munuo wakati kizungumza kwenye semina ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa soko la Ilala juu ya namna ya kutoa habari za unyanyasaji wa kijinsia kwa waandishi wa habari.
Aidha MUNUO ameeleza kuwa mifumo dume ya uongozi nchini imekuwa haitoi nafasi kwa wanawake kuwania uongozi kwenye masoko hali inayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake na Taifa kwa ujumla.