SERIKALI INATUMIA SH. 900 BILIONI KWA MWEZI KULIPA MADENI

SERIKALI INATUMIA SH. 900 BILIONI KWA MWEZI KULIPA MADENI

Like
277
0
Tuesday, 18 October 2016
Slider

Dodoma. Wakati wananchi wakilalamikia fedha kutoweka mifukoni, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatumia Sh900 bilioni kati ya Sh1.33 trilioni inazokusanya kila mwezi, kulipa madeni.

Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya nchini mjini hapa jana.

Kauli yake imekuja wakati kukiwa na mjadala kuhusu uchumi, baadhi ya watu kusema hali inazidi kuwa mbaya wakati taasisi za Serikali zikitoa takwimu zinazoonyesha kuwa uchumi uko imara.

Comments are closed.