SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA AFYA KUTOA ELIMU KWA MAKUNDI YALIYOKWENYE HATARI KUAMBUKIZWA VVU

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA AFYA KUTOA ELIMU KWA MAKUNDI YALIYOKWENYE HATARI KUAMBUKIZWA VVU

Like
244
0
Tuesday, 24 February 2015
Local News

SERIKALI imesema kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya kutoa elimu kwa makundi ya watu wanaotumia dawa za kulevya na wale wanaojihusisha na biashara ya ngono katika maeneo mbalimbali nchini ili kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI.Akizungumza kwa Niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dokta MOHAMED ALLY MOHAMED wakati wa kutambulisha matokeo ya tafiti za watu walio katika makundi maalum yaliyo katika hatari ya kuambukizwa Virusi vya Ukimwi katika mikoa 7 iliyofanyiwa utafiti ambayo ni Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Iringa, Mara, Tabora na Shinyanga.

Akitambulisha matokeo hayo Dokta MOHAMED amesema kuwa hali ya Maambukizi mapya miongoni mwa Wanaume na Wanawake katika maeneo yaliyofanyiwa utafiti imekuwa ikipungua kwa kasi ndogo licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kwa wadau mbalimbali kukabiliana na maambukizi hayo kutokana na makundi hayo kutobadili tabia.

AFYAYY

Picha ya pamoja ya washiriki hao baada ya uzinduzi wa chapisho.

AFYA4

Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akiwa ameshika chapisho lenye taarifa za utafiti kwa watu walio katika makundi maalum

AFYA

Comments are closed.