SERIKALI imesema imejidhatiti kuwalinda wananchi kwa kuzuia athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula kisicho salama kote nchini.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza ameyasema hayo na kufafanua kuwa uchafuzi wa chakula hufanya chakula kisiwe salama na hivyo kusababisha madhara ya kiafya ya muda mfupi na muda mrefu na hata vifo kwa mlaji pamoja na athari za kiuchumi.