MUUNGANO wa Taasisi zinazoshughulikia maradhi yasiyoambukiza Zanzibar –ZNCDA- umeishauri Serikali na Mashirika wahisani kuelekeza nguvu zao katika mapambano dhidi ya maradhi hayo kwani yamekuwa tishio kwa maisha ya wananchi kuliko maradhi mengine Zanzibar.
Mratibu wa –ZNCDA– Omar Abdalla Ali ametoa ushauri huo wakati wa zoezi la kuwapima afya wananchi wa shehia za Karakana, Chimbuni na Muembemakumbi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Omary amesema maradhi ya Shinikizo la damu, Kisukari na Saratani yamejitokeza na kuwa tishio kwa wananchi kutokana na uelewa mdogo walionao juu ya maradhi hayo na wengi kutokuwa na mwamko wa kupima afya zao.