Serikali – Uganda kupitia upya kodi ya mitandao ya kijamii

Serikali – Uganda kupitia upya kodi ya mitandao ya kijamii

Like
530
0
Thursday, 12 July 2018
Global News

Serikali ya Uganda imechukuwa hatua yakurekebisha sheria ambayo hivi karibuni ilianzisha kodi ya miamala ya kwenye simu na matumizi ya mitandao mingine ya kijamii.

Hatua hii inachukuliwa Jumatano wakati wananchi wakiandamana kupinga utozaji kodi huo na wakisema kuwa kodi hizo ni kadamizi na ni ghali mno.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa marekebisho ya muswada huo wa kodi wa 2018 ulipitishwa na Bunge na baadae ukapitishwa na rais na kuwa sheria iliyotungwa na bunge.

Sheria hiyo imeweka kodi ya shilingi 200 za Uganda ambayo inatozwa ili mtu aweze kutumia mitandao.

Rais Museveni amesema kodi ya miamala ya simu ipunguzwe kufikia asilimia 0.5 kutoka asilimia 1.

Lakini hapo awali Rais alikuwa amewafiki kodi hiyo ya mitandao itekelezwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *