SERIKALI ya Chile imetangaza hali ya dharura katika mji uliokumbwa na tetemeko la ardhi linaloaminika kuwa lenye nguvu zaidi.
Watu 11 wamepoteza maisha na wengine milioni moja wameacha makazi yao baada ya kutokea kwa tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha ritcha 8.3 kuleta athari siku ya Jumatano usiku.
Tetemeko hilo ambalo ndilo kubwa zaidi duniani na la sita kutokea nchini humo kwa kipindi cha mwaka huu lilidumu dakika tatu.