SERIKALI YA KENYA YATOA SHUKRANI KWA RAIS KIKWETE

SERIKALI YA KENYA YATOA SHUKRANI KWA RAIS KIKWETE

Like
182
0
Tuesday, 06 October 2015
Global News

SERIKALI ya Kenya imemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Jakaya mrisho Kikwete kwa kudumisha na kuboresha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Taarifa iliyotolewa  Ikulu Jijini Dar es salaam inaeleza kuwa shukrani za Kenya zimetolewa na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta katika mazungumzo aliyoyafanya na Rais Kikwete nchini humo.

Rais Kikwete yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu ambapo leo anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya Kenya.

Comments are closed.