SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMESHAURIWA KUFANYA JUHUDI KUWAHAMISHA OMBAOMBA

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMESHAURIWA KUFANYA JUHUDI KUWAHAMISHA OMBAOMBA

Like
229
0
Tuesday, 02 June 2015
Local News

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kufanya juhudi za kuwahamisha Ombaomba waliozagaa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mji wa Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza la Wawakilishi  WANU  HAFIDHI  AMEIR wakati akiwasilisha Maoni ya Kamati hiyo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

AMEIR amesema kuwa kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu wanaokaa katika Maeneo ya Mji wa Zanzibar na kuomba ni jambo ambalo halitoi taswira nzuri kutokana na Maadili ya Wananchi wa Zanzibar.

Comments are closed.