SERIKALI mpya ya mpito nchini Burkina Faso itakuwa na mkutano wa kwanza leo hii huku jeshi likishikilia nyadhifa muhimu Serikalini ikiwa ni Wiki tatu baada ya Jeshi kuchukuwa madaraka kufuatia kun’gatuka kwa Rais wa nchi hiyo kutokana na uasi wa umma.
Kiongozi mwenye nguvu jeshini Luteni Kanali ISAAC ZIDA ataendelea kushikilia wadhifa wa Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi.
Katibu Mkuu wa Serikali hiyo mpya ALAIN THIERRY OUATTARA ametangaza kwamba jeshi, pia litadhibiti Wizara ya mambo ya ndani.