SERIKALI YA WANAFUNZI UDSM YASIKITISHWA NA UTARATIBU WA UTOAJI MIKOPO

SERIKALI YA WANAFUNZI UDSM YASIKITISHWA NA UTARATIBU WA UTOAJI MIKOPO

Like
436
0
Wednesday, 04 November 2015
Local News

SERIKALI ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM imesema kuwa imesikitishwa na utaratibu wa kutoa mikopo uliofanywa na Bodi ya mikopo kufuatia asilimia 90 ya Wanafunzi kukosa mikopo ambapo jumla ya Wanafunzi 600 kati ya Wanafunzi zaidi ya elfu 7000 wanaodahiriwa katika chuo hicho ndio waliobahatika kupata mikopo hiyo.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Waziri wa Mikopo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Shitindi Venance amesema kuwa wameshangazwa na idadi ya mikopo iliyotolewa mwaka huu kuwa chini sana na kuwa baada ya kuwasilisha malalamiko yao kwa Bodi hiyo na kutorihishwa na majibu Wamepanga kwenda katika ngazi za juu kuwasiliana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Wizara ya Fedha.

Comments are closed.