SERIKALI YAAGIZA HALMASHAURI KUHAKIKISHA ELIMU INATOLEWA BURE

SERIKALI YAAGIZA HALMASHAURI KUHAKIKISHA ELIMU INATOLEWA BURE

Like
302
0
Monday, 21 December 2015
Local News

WIZARA ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi  imewataka wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmshauri za Wilaya, Miji na Manispaa zote nchini kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa agizo la utoaji wa elimu bure kwa shule za awali, msingi na sekondari kama lilivyotolewa na  rais.

Hatua hiyo imetokana na Wizara ya Elimu kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa elimu kuwa kuna baadhi ya walimuu wakuu wa shule za msingi na sekondari kuendelea kutoza fedha za uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza lakini pia kutoza michango kwa wazazi kwa muhula unaoanzia januari 2016 jambo ambalo ni kinyume na agizo la rais.

 

Comments are closed.